Mark 14

Shauri La Kumuua Isa

(Mathayo 26:1-5; Luka 22:1-2; Yohana 11:45-53)

1 aZilikuwa zimebaki siku mbili tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka, na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikuwa wakitafuta njia ya kumkamata Isa kwa hila na kumuua. 2 bLakini walisema, “Tusilifanye jambo hili wakati wa Sikukuu, maana watu wanaweza wakafanya ghasia.”

Isa Kupakwa Mafuta Huko Bethania

(Mathayo 26:6-13; Yohana 12:1-8)

3 cIsa alikuwa Bethania nyumbani kwa Simoni aliyekuwa na ukoma. Wakati alipokuwa ameketi mezani akila chakula cha jioni, mwanamke mmoja aliingia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya nardo
Nardo ni aina ya manukato yaliyotengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri.
safi ya thamani kubwa. Akaivunja hiyo chupa, akamiminia hayo manukato kichwani mwa Isa.

4Baadhi ya watu waliokuwepo pale walikuwa wakisemezana wao kwa wao, “Upotevu huu wote ni wa nini? 5Mafuta haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari
Dinari 300 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 300.
300, na fedha hizo wakapewa maskini.” Wakamkemea vikali huyo mwanamke.

6Lakini Isa akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mwanamke? Mwacheni! Yeye amenitendea jambo zuri sana. 7 fMaskini mtakuwa nao siku zote na mnaweza kuwasaidia wakati wowote mnaotaka. Lakini mimi hamtakuwa nami siku zote. 8 gHuyu mwanamke amenitendea lile aliloweza. Ameumiminia mwili wangu manukato ili kuniandaa kwa maziko yangu. 9 hAmin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.”

Yuda Akubali Kumsaliti Isa

(Mathayo 26:14-16; Luka 22:3-6)

10 iKisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, akaenda kwa viongozi wa makuhani ili kumsaliti Isa kwao. 11 jWalifurahi sana kusikia jambo hili na wakaahidi kumpa fedha. Hivyo yeye akawa anatafuta wakati uliofaa wa kumsaliti.

Isa Ala Pasaka Na Wanafunzi Wake

(Mathayo 26:17-25; Luka 22:7-14, 21-23; Yohana 13:21-30)

12 k lSiku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, siku ambayo kwa desturi mwana-kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wa Isa wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?”

13 mBasi akawatuma wawili miongoni mwa wanafunzi wake, akawaambia, “Nendeni mjini. Huko mtakutana na mwanaume amebeba mtungi wa maji. Mfuateni. 14 nMwambieni mwenye nyumba ile atakayoingia, ‘Mwalimu anauliza: Kiko wapi chumba changu cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka?’ 15 oAtawaonyesha chumba kikubwa ghorofani, kilichopambwa tena kilicho tayari. Tuandalieni humo.”

16 pWale wanafunzi wakaondoka na kwenda mjini, nao wakakuta kila kitu kama Isa alivyowaambia. Hivyo wakaiandaa Pasaka.

17 qIlipofika jioni, Isa akaja pamoja na wale wanafunzi wake kumi na wawili. 18 rWalipoketi mezani wakila, Isa akawaambia, “Amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti, mmoja anayekula pamoja nami.”

19Wakaanza kuhuzunika na kumuuliza mmoja baada ya mwingine, “Je, ni mimi Bwana?”

20 sAkawajibu, “Ni mmoja miongoni mwenu ninyi kumi na wawili, yule anayechovya mkate kwenye bakuli pamoja nami. 21 tMwana wa Adamu anaenda zake kama vile alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu huyo kama hangezaliwa.”

Kuanzishwa Kwa Meza Ya Bwana

(Mathayo 26:26-30; Luka 22:14-20; 1 Wakorintho 11:23-25)

22 uWalipokuwa wanakula, Isa akachukua mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi wake, akisema, “Twaeni mle; huu ndio mwili wangu.”

23 vKisha akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, nao wote wakanywa kutoka humo.

24 wAkawaambia, “Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. 25 xAmin, nawaambia, sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi siku ile nitakapounywa mpya katika Ufalme wa Mungu.”

26 yWalipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni.

Isa Atabiri Kuwa Petro Atamkana

(Mathayo 26:31-35; Luka 22:31-34; Yohana 13:36-38)

27 zIsa akawaambia, “Ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa: “ ‘Nitampiga mchungaji,
nao kondoo watatawanyika.’

28 aaLakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”

29 abPetro akasema, “Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.”

30 acIsa akamwambia, “Amin, nakuambia; leo, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, wewe mwenyewe utanikana mara tatu.”

31 adLakini Petro akasisitiza zaidi, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wale wengine wote wakasema vivyo hivyo.

Isa Aomba Katika Bustani Ya Gethsemane

(Mathayo 26:36-46; Luka 22:39-46)

32 aeWakaenda mahali paitwapo Gethsemane. Isa akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa, nami niende nikaombe.” 33Kisha akawachukua pamoja naye Petro, Yakobo na Yohana. Akaanza kuhuzunika sana na kutaabika. 34 afAkawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe.”

35 agAkaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba kwamba kama ingewezekana saa hiyo ya mateso imwondokee. 36 ahAkasema, “Abba,
Abba ni neno la Kiaramu ambalo maana yake ni Baba; ni mtoto wa kuzaa tu angeweza kulitumia kwa baba yake.
Baba, mambo yote yawezekana kwako. Niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo mimi, bali vile upendavyo wewe.”

37Akarudi kwa wanafunzi wake, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, “Simoni, umelala? Je, hukuweza kukesha hata kwa saa moja? 38 ajKesheni na mwombe, msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi, lakini mwili ni mdhaifu.”

39Akaenda tena kuomba, akisema maneno yale yale. 40Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. Nao hawakujua la kumwambia.

41 akAkaja mara ya tatu, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imewadia. Tazameni, Mwana wa Adamu anasalitiwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi. 42 alInukeni, twende zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!”

Isa Akamatwa

(Mathayo 26:47-56; Luka 22:47-53; Yohana 18:3-12)

43 amIsa alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili, akatokea. Alikuwa amefuatana na umati wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, na wazee.

44Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni, mkamchukue chini ya ulinzi.” 45 anMara Yuda akamjia Isa na kusema, “Rabi.”
Rabi ni neno la Kiebrania ambalo maana yake ni daktari, mwalimu au bwana. Walikuwa na madaraja matatu: La chini kabisa Rab (bwana), la pili Rabi (bwana wangu), na la juu kabisa Raboni (mkuu wangu, bwana wangu mkuu).
Akambusu.
46Wale watu wakamkamata Isa, wakamweka chini ya ulinzi. 47Ndipo mmoja wa wale waliokuwa wamesimama karibu aliuchomoa upanga wake na kumpiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio.

48 apKisha Isa akawaambia, “Mmekuja na panga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang’anyi? 49 aqSiku kwa siku nilikuwa pamoja nanyi nikifundisha Hekaluni, wala hamkunikamata. Lakini Maandiko sharti yatimie.” 50 arNdipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.

51Kijana mmoja, ambaye hakuwa amevaa kitu isipokuwa alijitanda nguo ya kitani, alikuwa akimfuata Isa. Walipomkamata, 52alikimbia uchi, akaliacha vazi lake.

Isa Mbele Ya Baraza La Wayahudi

(Mathayo 26:57-68; Luka 22:54-71; Yohana 18:13-24)

53 asWakampeleka Isa kwa kuhani mkuu, nao viongozi wa makuhani wote, na wazee na walimu wa sheria wote wakakusanyika pamoja. 54 atPetro akamfuata kwa mbali, hadi uani kwa kuhani mkuu. Huko akaketi pamoja na walinzi, akiota moto.

55 auViongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi
Baraza la Wayahudi hapa ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa ndilo baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi, lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.
lote wakatafuta ushahidi dhidi ya Isa ili wapate kumuua. Lakini hawakupata jambo lolote.
56Wengi walitoa ushahidi wa uongo dhidi yake, lakini maelezo yao hayakukubaliana.

57Ndipo wengine wakasimama wakatoa ushahidi wa uongo dhidi yake, wakisema: 58 aw“Sisi tulimsikia akisema, ‘Mimi nitalibomoa Hekalu hili lililojengwa na wanadamu, na katika siku tatu nitajenga jingine ambalo halikujengwa na wanadamu.’ ” 59Lakini hata hivyo, ushahidi wao haukukubaliana.

60 axBasi kuhani mkuu akasimama mbele yao, akamuuliza Isa, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?” 61 ayLakini Isa akakaa kimya, hakusema neno lolote.

Kuhani mkuu akamuuliza tena, “Je, wewe ndiwe Al-Masihi,
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.
Mwana wa Mungu Aliyebarikiwa?”

62 baIsa akajibu, “Mimi ndimi. Nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.”

63 bbKuhani mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? 64 bcNinyi mmesikia hayo makufuru. Uamuzi wenu ni gani?”

Wote wakamhukumu kwamba anastahili kifo.
65 bdKisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate; wakamfunga kitambaa machoni, wakampiga kwa ngumi na kumwambia, “Tabiri!” Walinzi wakamchukua na kumpiga makofi.

Petro Amkana Isa

(Mathayo 26:69-75; Luka 22:56-62; Yohana 18:15-18, 25-27)

66 bePetro alipokuwa bado yuko chini kwenye ua wa jumba la kifalme, tazama akaja mmoja wa watumishi wa kike wa kuhani mkuu. 67 bfAlipomwona Petro akiota moto, akamtazama sana, akamwambia,

“Wewe pia ulikuwa pamoja na Isa, Mnasiri.”

68 bgLakini Petro akakana, akasema, “Sijui wala sielewi unalosema.” Naye akaondoka kuelekea kwenye njia ya kuingilia.

69 bhYule mtumishi wa kike alipomwona mahali pale, akawaambia tena wale waliokuwa wamesimama hapo, “Huyu mtu ni mmoja wao.” 70 biLakini Petro akakana tena.

Baada ya muda kidogo wale waliokuwa wamesimama hapo karibu na Petro wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya!”
71 bjPetro akaanza kujilaani na kuwaapia, “Mimi simjui huyu mtu mnayesema habari zake!”

72 bkPapo hapo jogoo akawika mara ya pili. Ndipo Petro akakumbuka lile neno Isa alikuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akavunjika moyo, akalia sana.
Copyright information for SwhKC